technology

Hofu ya Ebola Nigeria, aliyekufa Calabar ashukiwa

Hofu ya Ebola Nigeria, aliyekufa Calabar ashukiwaHofu ya kuibuka tena homa hatari ya Ebola imetanda kusini mwa Nigeria ikiwa ni mwaka mmoja sasa tangu nchi hiyo itangaze kutokuweko tena homa hiyo katika nchi hiyo. Wasiwasi huo unatokana na ripoti zinaoonesha kuwepo kwa mlipuko mpya wa homa hatari ya Ebola katika mji wa Calabar kusini mwa Nigeria. Shirika la usimamizi wa mambo ya dharura nchini Nigeria linasema kuwa, watu kumi wamewekewa karantini baada ya kugusana na mtu aliyeonekana kuwa na dalili za homa hiyo. Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa, mtu huyo alifariki dunia muda mchache tu baada ya kufikishwa hospitalini.
Kwa sasa wataalamu wa afya nchini Nigeria wanazifanyia majaribio na utafiti sampuli za damu ya mtu huyo aliyeaga dunia. Siku ya Jumatano iliyopita Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuwa, nchi tatu zilizokuwa zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo ambazo ni Guinea, Sierra Leone na Liberia, zimeweza kuwa na wiki yake ya kwanza bila kuwa na kesi yoyote ya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola tokea mlipuko wa ugonjwa huo uanze mwezi Machi mwaka 2014. Zaidi ya watu elfu kumi na moja walifariki dunia kwa ugonjwa huo wengi wao wakiwa ni kutoka katika nchi hizo tatu za magharibi mwa Afrika.

chanzo-tehran radio
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :