Muuzaji madawa ya kulevya mtoro akamatwa Brazil
Polisi nchini Brazil wamemkamata mmoja wa walanguzi wakubwa zaidi wa madawa ya kulevya nchini humo.
Mario Sergio Machado Nunes, ambaye pia anafahamika kama "O Goiano" amekuwa mafichoni tangu atoroke jela miaka miwili iliyopita.Polisi wanasema kuwa alifanyiwa upasuaji ili kubadili umbo lake na alikuwa akitumia stakabadhi bandia.
Guianio alikamatwa akiwa katika jumba moja la kifahari katika mji wa pwani wa Guajura.
Hapo jana, maafisa wa kupambana na mihadarati walitangaza kiinua mgongo cha dola milioni 5 kwa mtu yeyote atakayetoa habari zitakazopelekea kukamatwa kwa kiongozi wa genge la wauazaji mihadarati Joaquin Chapo Guzman ambaye kama Goiano alitoroka gerezani.
chanzo-bbcswahili.com
Labels
MICHEZO
Post A Comment
Hakuna maoni :