technology

Al Shabab yauteka mji mwingine Somalia

Al Shabab yauteka mji mwingine Somalia Wanamgambo wa kitakfiri wa al Shabab wameuteka mji mwingine katikati mwa Somalia kufuatia kuondoka katika eneo hilo vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika nchini Somalia(AMISOM). Sheikh Abdiasis Abu Musab Msemaji wa al Shabab amesema kuwa wameuteka mji wa Buqda kwa amani. Wanajeshi wa AMISOM ambao waliuteka mji wa Buqda kutoka kwa wanamgambo wa al Shabab katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja uliopita, waliondoka katika mji huo juzi usiku. Kwa upande wake afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Somalia amesema kuwa wanajeshi wa AMISOM waliondoka katika mji huo ili kukabiliana na al Shabab katika maeneo mengine na kwamba watarudi huko baadaye.
Huu ni mji wa tatu kuanguka mikononi mwa wanamgambo wa kitakfiri wa al Shabab tangu Ijumaa

(tehranradio)
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :