technology

Wakati Baba wa mtoto aliyekufa akataa hifadhi huku Picha ya mtoto Aylan Kurdi yamliza waziri wa Sweden

Picha ya Aylan Kurdi yamliza waziri wa Sweden
Picha ya maiti ya mkimbizi mtoto Aylan Kurdi wa Syria iliyopatikana katika pwani ya Uturuku imemtoa machozi Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden, Margot Wallström, ambaye amesema kuwa picha hiyo inaakisi maafa na masaibu ya watu wanaokimbia vita katika nchi za Syria na Iraq.
Waziri Margot alitokwa na machozi baada ya kuoneshwa picha ya Alyan aliyesombwa na mawimbi bahari akiwa na wazazi wake waliokuwa wakijaribu kukimbilia Ulaya wakitolea Syria. "Picha hii imetuathiri na kuakisi masaibu ya wakimbizi", amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden. Ameongeza kuwa picha ya maiti ya mtoto huyo imewahimiza walimwengu kuchukua hatua kubwa zaidi kuhusu mgogoro wa wakimbizi barani Ulaya. Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden amezitaka nchi zote za Ulaya kutekeleza majukumu yao kuhusu mgogoro huo.
Picha ya maiti ya mtoto mchanga, Aylan Kurdi, aliyekuwa na umri wa miaka mitatu akiwa amelala kwenye mchanga kwenye pwani ya Aegean kusini magharibi mwa Uturuki imewahuzunisha sana walimwengu baada ya kuchapishwa katika kurasa za mitandao ya kijamii na baadaye magaztini na koneshwa kwenye runinga.

(chanzo tehran idhaa ya kiswahili)
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :