Sikia hii kutoka kwa mugambe!!!!Mali ya serikali ya Zimbabwe yapigwa mnada

Nyumba inayomilikiwa na serikali ya Zimbabwe imeuzwa $280,000 (£180,000) kupitia mnada Afrika Kusini.
Mwekezaji
katika nyumba Arthur simatakopoulos amenunua nyumba hiyo iliyoko mji
wa Cape Town, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Mohammed Allie.
Mnada
huyo umefanyika baada ya serikali hiyo kushindwa kwenye vuta nikuvute
iliyodumu miaka mitano na shirika la kutetea haki za Waafrikaner nchini
Afrika Kusini kwa jina AfriForum.
Shirika hilo liliitaka serikali
ya Zimbabwe kulipa gharama ya kesi baada ya serikali hiyo kushindwa
kwenye kesi iliyohusu mageuzi ya umiliki wa mashamba.
Serikali ya Zimbabwe chini ya Rais Robert Mugabe ilikuwa imechukua mashamba kutoka kwa Wazungu na kuyapa Waafrika weusi.
Mahakama
maalum ya muungano wa mataifa ya Afrika Kusini (Sadc) iliamua 2008
kwamba mpango huo ulikuwa kinyume cha sheria, shirika hilo lilisema.
Mahakama Kuu mjini Pretoria iliwaagiza maafisa nchini Afrika Kusini kutwaa mali hiyo 2010.
Zimbabwe ilifika kortini mara kadha kupinga uamuzi huo bila mafanikio.
chanzo-bbcswahili.com
Labels
AFRIKA
Post A Comment
Hakuna maoni :