2 Face awaomba D’banj na Don Jazzy kuyamaliza, D’banj kajibu hivi.
Muimbaji mkubwa kutoka Nigeria aliyesheherekea kufikisha miaka 40 weekend hii ametumia siku hio kubadilisha maisha ya wengi kwa kutoa ushauri kwa vijana na kuleta pamoja wasanii wasioelewana na kujaribu kuwapatanisha.
2Face Idibia ametumia birthday yake kuwaomba watu wakubwa kwenye muziki D’banj aka Kokomaster na producer Don Jazzy kuyamaliza mambo yao na kufanya kazi tena.
2Face aliongea jambo hili kwenye jukwa na kusema yeye ni shabiki mkubwa wa kazi zao. Kwenye show hio walikuwepo wote wawili D’Banj na Don Jazzy
D’Banj aliimba ‘I’m Feeling Good’ wimbo uliotayarishwa na Don Jazzy Ft 2Face.
D’Banj alipanda kwenye jukwaa na kusema “mambo mazuri wanayopitia wasanii wa Marvin kama Korede Bello, Reekado Banks na Di’Ja yalitolewa jasho na yeye na Don Jazzy, wanapata umaarufu na kujulikana kwa mgongo wa Don Jazzy bila kuteseka so inabidi wajitume zaidi“.
Labels
burudani
Post A Comment
Hakuna maoni :