Huu ndio Ubunifu mwingine katika dunia ambao hauja wahi kutokea.......

Juu ya Milima ya Kronplatz iliyoko Jimbo la South Tyrol, Italy.. hii ni moja ya vivutio vya aina yake kabisa, ni ubunifu wa Mhandisi Zaha Hadid.

Picha ya Juu ya Milima hiyo ndani ya Italy.
Juu ya Kilele cha Mlima Mkubwa Afrika ambao uko Tanzania, Mlima Kilimanjaro
kuna theluji ambayo ni ya asili kabisa na ni kivutio kikubwa
kinachofanya Watalii wengi wakitajiwa Mlima Kilimanjaro basi moja ya
vitu vya kuvutia wanavyotamani kuviona ni ile theluji juu ya Mlima.
Pata picha unapanda juu ya Milima
kutalii alafu unakutana na Mijengo ya Makumbusho ambayo ndani yake kuna
vitu vingine pia vya kukuvutia uendelee kutalii.
Nimezipata pichaz nje mpaka ndani ya Jumba la Makumbusho lililopewa jina la Messner Mountain Museum, kilichomo
humo ni michoro ya kuvutia ambapo mbunifu wa Mjengo anasema hakuna kitu
cha Sayansi wala maonesho ya sanaa ndani yake, ni michoro inayohusu
masuala ya binadamu na Milima, basi !!





Huu ndio muonekano mwingine wa muundo wote wa Mjengo wenyewe nje mpaka ndani.
Labels
SIYO YA KAWAIDA
Post A Comment
Hakuna maoni :