Majaji 34 Ghana kuhojiwa kwa kula rushwa

Kwa mjibu wa aliyeitengeneza kanda hiyo yenye urefu wa takribani saa mia tano, ilirekodiwa kwa zaidi ya miaka miwili. Ni majuma mawili sasa tangu Jaji Mkuu wa Ghana alipokabidhiwa nakala yake.
Rekodi hiyo inaonyesha majaji wa mahakama ndogo na za juu wakichukua hongo na kuwalazimisha wenye kesi kutoa pesa.
Anes, Mwandishi wa habari za uchunguzi, ambaye pia ni mwanasheshia aliwafuata majaji kuwapa hongo ili wawaachie huru watuhumiwa. Katika maeneo mengine alijifanya mwenye kushitaki ili atoe hongo. Leo, chombo kinachohusika na kuwaadhibu wanasheria wanaolalamikiwa kwa rushwa kitawasikiliza majaji wote 34 wanaohusishwa na kashifa hiyo.
Tuhuma za rushwa si mpya katika mahakama za nchini Ghana lakini ambacho kimekuwa kikikosekana ni ushahidi madhubuti. Kwa Waghana wengi, uchunguzi huu wa sasa ni ushahidi mzuri wa kuunga mkono malalamiko yao ya muda mrefu juu ya rushwa katika mahakama.
Mwandishi huyo wa habari za uchunguzi anapanga kuiachia video hiyo katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Ghana mwezi ujao.
chanzo-bbcswahili.com
Labels
kimataifa
Post A Comment
Hakuna maoni :