Walemavu wa macho kupiga kura wenyewe

Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania,
watu wenye ulemavu wa macho watashiriki katika kumchagua kiongozi
wanayemtaka kwa kutumia kifaa maalum chenye maandishi ya nukta nundu au
Braille katika uchaguzi mkuu utakofanyika Oktoba 25 waka huu.
Vifaa
hivyo vitaanza kufanyiwa majaribio mwishoni mwa mwezi huu ambapo watu
hao wataweza kufundishwa jinsi ya kupiga kura bila ya kuwa na mtu wa
kumsaidia au kumwongoza kupiga.Kumekuwa na madai kuwa wale waliokuwa wakiwasaidia watu wenye ulemavu wa kuona mara nyingi huwapotosha walemavu hao kwa kupiga kura kinyume ya matarajio ya mlemavu huyo.
Tangu jadi walemavu wa macho wamekuwa wakishiriki katika kupiga kura kwa kusaidiwa na watu ambao huwa wanenda nao katika vituo vya wa kupigia kura kwa lengo la kuwaelekeza wakati mwingine husaidiwa na mawakala au wasimamizi wa vituo vya kupigia kura.
bbc.com/swahili/habari
Labels
KITAIFA
Post A Comment
Hakuna maoni :