Uchumi wa zimbabwe unadidimia ;IMF
Shirika la fedha duniani IMF limesema hali ya uchumi nchini Zimbabwe imezidi kudidimia.
Aidha IMF inasema kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi huo ni wa kiwango cha chini mno kuliko vile ilikuwa imekadiriwa.
Hayo yametokea baada ya vuta ni kuvute baina ya serikali na sekta ya kibinafsi huku serikali ikitaka kuimarisha sekta ya uchumi na kutaifisha soko la ajira.

Serikali ilikuwa imeruhusu kupunguzwa kwa idadi ya wafanyikazi wake lakini sekta ya umma ilipotaka kuiga mfano ikazua hofu ya kupotezwa kwa nafasi za ajira.
Rais Robert Mugabe na chama chake zanu- PF kimekuwa kikiongoza nchi ya Zimbabwe katika njia yake mwenyewe.
chanzo- bbc.com/swahili/habari
Labels
kimataifa
Post A Comment
Hakuna maoni :