HII NI HATUA NYENGINE tangu wanafunzi 43 kutoweka Mexico Mwaka 1 upite.

Mwaka mmoja uliopita, wanafunzi 43 walipotea katika mji wa Iguala katika jimbo la Guerrero, kusini mwa Mexican.
Maelfu
ya watu wanashiriki katika maandamano makubwa katika mji mkuu wa Mexico
kuadhimisho mwaka mmoja tangu kutokea kwa kisa hicho.
Uchunguzi
wa serikali ulidai kuwa, wanafunzi hao walikabidhiwa kwa genge moja la
uhalifu, ambao waliwauwa na kisha kuteketezwa mabaki ya maiti yao katika
eneo la urushwaji taka.

Ripoti hiyo haijakataliwa tu na jamaa ya wanafunzi
hao, bali pia ripoti kutoka kwa kundi moja la wataalamu wa uchunguzi
huru, hivi majuzi ilihoji uhalali wa ripoti hiyo ya uchunguzi wa
serikali.
Bernardo Santos Campos, babake Hose Angel, Ameiambia BBC
kuwa wazazi wa wanafunzi hao waliotoweka hawatasitisha maandamano
kamwe, hadi watakapojua kilichofanyika.

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, ameahidi uchunguzi upya ufanywe.
Kesi
hiyo ni nembo ya kutoweka kwa maelfu ya raia wa Mexico, ambao
wametoweka katika muongo mmoja wa ghasia inayohusisha makundi hasimu ya
ulanguzi wa dawa za kulevya na walinda usalama.
chanzo-bbcswahili.com
Post A Comment
Hakuna maoni :