Mashambulio ya Saudia yameua watoto 500 Yemen
Watoto
wapatao 505 wameuawa nchini Yemen kufuatia hujuma za ndege za kivita za
Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo masikini zaidi katika ulimwengu wa
Kiarabu.
Kwa mujibu wa taarifa ya
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNCEF, watoto wengine 702
wamejeruhiwa katika uvamizi huo wa Saudi Arabia na waitifaki wake dhidi
ya Yemen. UNICEF aidha imesema vijana milioni 1.7 Yemen wanakabiliwa na
hatari ya lishe duni huku nchi hiyo ikielekea kutumbukia katika maafa
makubwa ya binadamu. UNICEF katika ripoti hiyo ya Ijumaa imesema watoto
milioni 1.2 walio chini ya umri wa miaka mitano nchini Yemen wamekumbwa
lishe duni. Kwa ujumla ni kuwa karibu watoto na mabarobaro milioni 10
Yemen, ambao ni asilimia 80 ya watu wa nchi hiyo, wanahitajia misaada
ya dharura ya kibinadamu. Saudi Arabia ilianza kuishambulia Yemen
tarehe 26 Machi mwaka huu kwa lengo la kuiondoa madarakani harakati ya
Ansarullah. Mashambulizi hayo ya Saudia yameua Wayemen wasio na hatia
zaidi ya 6,000 wengi wao wakiwa ni raia hasa wanawake, watoto wadogo na
wazee. Saudia pia imedondosha mabomu katika misikiti, shule, viwanda na
mahospitali katika maeneo mbalimbali ya Yemen.
(chanzo-tehran radio)
Post A Comment
Hakuna maoni :