kutunishiana misuli bado kunaendelea kati ya Putin na obama juu ya mgogoro wa syria
Matamshi hayo ya msemaji wa ikulu ya Russia yametolewa ikiwa zimepita siku mbili baada ya ikulu ya Marekani (White House) kusema katika taarifa yake kuwa ni muhimu kuunda serikali mpya huko Syria bila ya Assad. Naye Yury Ushakov Mshauri wa ngazi ya juu wa Rais Putin amesema kuwa, viongozi wa sasa wa Syria ni moja ya nguvu imara na madhubuti katika mapambano dhidi ya wanamgambo wa Daesh. Rais Putin wa Russia aliahidi kuendelea kuiunga mkono serikali ya Syriana wananchi katika mapambano yao dhidi ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh kupitia mazungumzo aliyofanywa tarehe 29 mwezi uliopita na Walid al Muallem Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria aliyekuwa ziarani nchini Russia.
(chanzo tehran radio idhaaa ya kiswahili.com)
Post A Comment
Hakuna maoni :