
Zaidi ya wanajeshi 40 wa Yemen wameuawa kufuatia shambulio la
anga la Saudi Arabia dhidi ya kituo kimoja cha jeshi katika mji wa
Hadhramaut katikati mwa nchi hiyo. Aidha vyombo vya habari vya Yemen
vimeripoti kuwa, zaidi ya wanajeshi 200 wa Saudia wamejeruhiwa katika
shambulio hilo. Wakati huo huo vikosi vya Yemen vikisaidiwa na kamati za
wapiganaji za wananachi limerusha makombora na kukilenga kituo cha
kijeshi cha vikosi vya Saudia katika mji wa Dhahran al-Janub na
kuvisababishia vikosi hivyo hasara kubwa. Hayo yanajiri katika hali
ambayo, hali ya kibinadamu nchini Yemen inaripotiwa kuwa mbaya mno hasa
katika kipindi hiki cha funga ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na
kukosekana huduma na mahitaji muhimu ya maisha. Umoja wa Mataifa
umetangaza kuwa, zaidi ya Wayemeni 3,000 wameuawa na wengine zaidi ya
14,000 wamejeruhiwa tangu Saudi Arabia ilipoanzisha mashambulizi yake ya
kichokozi nchini humo miezi mitatu
Post A Comment
Hakuna maoni :