Wanajeshi 50 wa Saudia wauawa nchini Yemen
Wanajeshi wa Yemen wamewaangamiza askari 50 vamizi wa Saudia Arabia ambao walikuwa wameweka kambi yao katika mkoa wa Ma’rib.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mkoa huo wa kati mwa Yemen, wanajeshi hao wamelengwa katika fremu ya mashambulio ya Wayemen ya kulipiza kisasi hujuma za kijeshi na jinai zinazotekelezwa na utawala vamizi wa Saudia dhidi ya Yemen.
Jeshi la Yemen pia limetekeleza oparesheni katika wilaya ya al-Khobe katika mkoa wa Jizan kusini magharibi mwa Saudi Arabia. Ripoti zinasema wanajeshi watano Wasaudi wameuawa katika shambulizi hilo. Aidha wanajeshi wengine watano wa Saudi Arabia wameripotiwa kuuawa katika shambulizi la vikosi vya Yemen huko Asir kusini magharibi mwa ufalme huo.
Kwingineko Jumatano asubuhi, ndege za kivita za Saudia zilitekeleza hujuma saba mjini Sirwah, yapata kilomita 120 kutoka mji mkuu wa Yemen, Sana’a.
Labels
AFRIKA
Post A Comment
Hakuna maoni :