technology

KURA YA MAONI yasababisha Kongo kusitishi huduma ya intaneti, yafunga Radio ya Ufaransa

Kongo yakatia intaneti, yafunga Radio ya Ufaransa Serikali ya Kongo Brazzaville imekata intaneti sambamba na kufunga mawimbi ya radio ya kimataifa ya Ufaransa RFI nchini humo. Aidha kati ya hatua zingine zilizochukuliwa na wakuu wa Brazzaville ni kusimamisha huduma zote za ujumbe mfupi wa simu SMS. 

Hatua hizo zimechukuliwa siku moja baada ya watu wanne kuuawa mjini Brazzaville katika makabiliano baina ya vikosi vya usalama na wafuasi wa upinzani wanaopinga kura ya maoni kuhusu katiba mpya. 

Wapinzani Jamhuri ya Kongo wanaandamana wakipinga vikali kura ya maoni ya katiba mpya ambayo inampa Rais Dennis Sassou Nguesso uwezo wa kugombea tena urais nchini humo katika uchaguzi wa mwaka 2016. Kwa mujibu wa katiba ya sasa, Sassou Nguesso mwenye umri wa miaka 72 hawezi kugombea urais. 
Aidha kwa mujibu wa katiba iliyoko hawezi kugombea urais kwa sababu amemaliza mihula yake miwili. Hata hivyo katika katipa mpya iliyopendekezwa vizingiti hivyo viwili vimeondolewa. Waungaji mkono wa Sassou Nugesso pia wamejitokeza mitaani mjini Brazzaville kuunga mkono marekebisho ya katiba. Sassou Nguesso aliye na umri wa miaka 72, alikuwa rais tangu mwaka 1979 hadi 1992. Baadaye Nguesso alihudumu kama kiongozi wa upinzani na kurejea tena madarakani baada ya kujiri vita vifupi vya ndani nchini humo mwaka 1997, baada ya vikosi vyake vya uasi kumng'oa madarakani rais wa wakati huo Pascal Lissouba.
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :