FIFA: Blatter asalia Kimya !
Rais wa FIFA Sepp Blatter
anatarajiwa kuonekana hadharani kwa mara ya kwanza siku moja baada ya
maafisa wakuu wa shirikisho hilo kukamatwa kufuatia tuhuma za ulaji
rushwa.Kwa kawaida Blatter huwa anawahutubia wajumbe na kuwakaribisha lakini kufikia sasa tayari imeshabainika kuwa
Blatter ambaye uongozi wake unatuhumiwa kwa kuendeleza ulaji rushwa na mlungula hatohudhuria hafla ya madaktari na wanakamati.
JACK WARNER
Msemaji wa shirikisho hilo amesema kuwa ni wazi kwanini Blatter hatohutubia.
Wakati hayo yakijiri aliyekuwa makamu wa Blatter, Jack Warner amekesha kizuizini Trinidad and Tobago baada yake kujisalimisha kwa polisi.
Kitita hicho kilikuwa kiinua mgongo chake baada ya Afrika Kusini kupewa uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2010.
Warner amepinga kufanya kosa lolote sawa na shirikisho la soka la Afrika Kusini.
BRAZIL
Huko Brazil polisi mjini Rio de Janeiro wamevamia afisi za kampuni moja ya mauzo inayosadikika kuwa na ushirika wa karibu na kampuni ya Traffic inayoshtumiwa kwa kufaidi zabuni za kandarasi za FIFA bila kufuata kanuni za utoaji zabuni.
Afisa mkuu katika kampuni hiyo Klefer Sports Marketing,bwana Kleber Leite amekanusha madai dhidi ya kampuni hiyo akisema kuwa atashirikiana na maafisa wanaoendesha uchunguzi huo.
WADHAMINI WAKUU
Siku moja tu baada ya maafisa wa kitengo cha FBI kupendekeza kushtakiwa kwa maafisa wakuu 14 wa shirikisho la soka duniani FIFA,
mdhamini mkuu wa FIFA kampuni ya VISA sasa imeonya kuwa huenda ikalazimika kutathmini upya uhusiano baina yake na FIFA hususan kufuatia kukamatwa kwa maafisa 11 kwa madai ya ufisadi.
Wadhamini wengine Coca-Cola, Hyundai na Adidas pia wamelezea kutoridhishwa kwao na jinsi mambo yanayvoendeshwa katika FIFA.
Kampuni ya kutengeza magari ya Hyundai, imelezea kushtushwa na madai dhidi ya maafisa wakuu wa FIFA.
Post A Comment
Hakuna maoni :