Askari na nchi kuenziwa katika siku ya kimataifa ya walinda amani wa UM
Kuelekea siku ya kimataifa ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa hapo
kesho Katibu mkuu Ban Ki-moon katika ujumbe wake pamoja na mambo mengine
ametaka nchi wanachama kutoa ushirikiano wa kifedha na askari katika
vikosi vya kulinda amani akisisitiza kuwa operesheni za kulinda amani
lazima zifanyike kisasa na kiteknolojia zaidi.
Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu wa Ofisi ya Kijeshi ya Idara
ya Ulinzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa, DPKO, Brigedia Jenerali Ahamed
Mohammed amesema kuelekea siku hii adhimu maandalizi yanaendelea ambapo
pamoja na mambo mengine ametaja mambo yatakayofanyika ikiwa nisehemu ya
kuwaenzi walinda amani waliopoteza maisha na wale wanaoendelea na zoezi
hilo.
Katika mahojiano maalum na idhaa hii mjini New York
Brigedia Jenerali Mohammed anasema hafla tatu muhimu zitafanyika ikiwamo
kuweka shada la maua ili kuwaenzi walinda amani waliopoteza maisha
Post A Comment
Hakuna maoni :