vita mpya kati ya Jose Mourinho na Arsene Wenger baada ya kukiri hadharani kuwa anataka Arsenal itolewe Ligi ya Mabingwa [Uefa].

The Gunners walijipa uhai katika michuano hiyo baada ya kuifunga Dinamo Zagreb Jumanne.
Kikosi hicho cha Wenger bado kinaweza kutinga hatua ya mtoano iwapo kitaifunga Olympiakos kwa magoli mawili bila mjini Athens, au kufikia ushindi wa 3-2 Wagiriki hao waliopata wakiwa Emirates.
Lakini Mourinho, baada ya kuiona Chelsea ikiendelea kushamiri katika michuano hiyo baada ya kushinda 4-0 ugenini dhidi ya Maccabi Tel Aviv, anatumai Wagiriki hao watakuwa pigo kwa Wenger.
Akisisitiza kuwa si rahisi kwa klabu hiyo ya Uingereza [Arsenal] kusonga, bosi huyo wa Chelsea alibainisha kuwa atakwenda kinyume na Arsenal.
Alisema: "Wapo [Arsenal] kwenye kundi ambalo rafiki yangu mtoto Marco Silva ni meneja wa Olympiakos.
"Itapendeza Marco atafanikiwa kuendelea hatua nyingine, nataka kuwa wazi kabisa na nasema ningependa Olympiakos iendelee."
Tofauti na kutaka Mreno mwenzake Silva kusonga mbele ya Wenger, Jose Mourinho anatafakari pia kuhusu majeraha aliyopata John Terry katika ushindi waliopata Israel baada ya kuumia kifundo cha mguu.
Kama vipimo vitaonyesha ameumia sana, Chelsea watalazimika kucheza mechi sita bila ya nahodha wao mwezi Desemba - kuanzia mechi dhidi ya Spurs ugenini Jumamosi.
Lakini beki mwenza wa Terry, Gary Cahil amesisitiza kuwa hakuna kitakachoizuia Chelsea kushinda mechi za michuano yote.
"Ni vema kuendeleza mapambano kwa kasi tuliyoianzisha," alisema Cahill. "La kwanza na la msingi zaidi ni Ligi ya Mabingwa na kuhakikisha tunafanya kila liwezekanalo kumaliza hatua ya makundi tukiwa vinara.
Labels
MICHEZO
Post A Comment
Hakuna maoni :