technology

Waasi Sudan Kusini watishia kuanzisha vita

Waasi Sudan Kusini watishia kuanzisha vitaWaasi wa Sudan Kusini wametishia kuanzisha tena mapigano nchini humo.Waasi hao wametishia kuwa iwapo serikali ya nchi hiyo itazidisha mara tatu mikoa ya nchi hiyo kinyume na makubaliano ya amani yaliyofikiwa, basi wataanzisha mapigano nchini humo. 

Mabior Garang msemaji wa waasi  hao amesema kuwa, serikali ya Juba imeandaa mazingira ya kuigawa mikoa ya Sudan Kusini kwa mujibu wa ukabila na asili, kwa mpango wake huo uliokusudia wa  kuzidisha mara tatu mikoa ya nchi hiyo. 

Garang amesema, vita vitaanza tena Sudan Kusini iwapo serikali ya nchi hiyo itaifanya mikoa ya nchi hiyo kuwa  mara tatu ya idadi yake ya sasa. 

Makubaliano yaliyosainiwa tarehe 26 Agosti mwaka huu kati ya serikali ya Juba na waasi kwa ajili ya kurejesha amani na kusimamsha mapigano, yanajumuisha suala la kugawana nyadhifa za serikali katika mikoa kumi inayounda nchi hiyo mpya.


chanzo-tehran radio
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :