technology

Mahujaji wa Tanzania walioaga dunia Mina wafikia 11

Mahujaji wa Tanzania walioaga dunia Mina wafikia 11Serikali ya Tanzania imepokea majina matatu ya Mahujaji wengine wa nchi hiyo waliofariki dunia katika maafa ya Mina kutokana na tukio la msongamano na mkanyagano lilitokea wakati wa kutekelezwa ibada ya Hija mwaka huu huko Saudi Arabia. Taarifa ya serikali ya Tanzania imeelesa kuwa, imepokea majina mengine matatu na hivyo , kufanya idadi ya Mahujaji wa Tanzania waliopoteza maisha katika maafa ya Mina kufikia 11. Hayo yalithibitishwa jana na Serikali kupitia taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari. Taarifa hiyo iliwataja watatu zaidi waliofariki dunia katika maafa ya Mina kuwa ni Yusuf Ismail Yusuf kutoka kikundi cha Khidmat Islamiya, Rahma Salim Suweid kutoka kikundi cha Ahlu Daawa na Issa Amir Faki. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Mahujaji hao walitambuliwa baada ya kupitia taarifa zao za vidole zilizotolewa na Serikali ya Saudi Arabia. Serikali ya Tanzania imesema, ubalozi wake mjini Riyadh unaendelea kufuatilia orodha mpya ya taarifa za vidole, iliyotolewa na serikali ya Saudi Arabia kwa ajili ya kuwabaini Mahujaji wa Tanzania ambao hawajatambuliwa. Mpaka sasa zaidi ya mahujaji 30 wa Tanzania hawajulikani walipo. Hayo yanjiri huku Saudia ikiendelea kulaumiwa kutokana na maafa ya Mina. Zaidi ya Mahujaji 4,000 walipoteza maisha katika maafa ya Mina yaliyotokea Septemba 24 wakati wa ibada ya Hija.
chanzo-tehran radio
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :