Volkswagen kurekebisha magari yake
Kampuni ya magari ya Volkswagen imesema magari yake yaliayoathirika na sakata ya gesi chafu yatafanyiwa marekebisho.
Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo ya magari, Mathias Mueller amesema magari hayo yanatarajiwa kurudishwa ili kufanyiwa marekebisho kuanzia mwaka ujao.
Ameliambia gazeti moja nchini ujerumani kuwa mengi ya magari millioni 11 yanayotumia mafuta ya diesel yatafanyiwa marekebishi kidogo ya mitambo
chanzo-bbcswahili.com
Post A Comment
Hakuna maoni :