technology

Nyepesi nyepesi mchana huu!!!!!!!Hoteli walimo viongozi vibaraka Aden, yashambuliwa

Hoteli walimo viongozi vibaraka Aden, yashambuliwaDuru za kuaminika kutoka Aden, Yemen zimearifu kushambuliwa hoteli ya al-Qasr ambayo anaishi ndani yake Khaled Bahah, Waziri Mkuu wa Yemen anayeungwa mkono na Saudi Arabia, mapema leo asubuhi. Kwa mujibu wa mashuhuda, makombora manne mazito yameitikisa hoteli hiyo ambapo kumeshuhudiwa moto mkubwa ukipaa katika jengo hilo. Aidha mashuhuda wameeleza kuonekana ndege za Saudi Arabia zikizunguka eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada kwa maafisa wa Saudia na viongozi vibaraka wa Yemen waliokuwa wakiishi hotelini hapo. Baadhi ya vyombo vya habari vya Kiarabu vimetangaza kuwa, Bahah na baadhi ya mawaziri wamesalimika katika shambulizi hilo lililotekelezwa na jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati za wananchi nchini humo. Wakati huo huo mwandishi wa kanali ya televisheni ya Russia Today amethibitisha kuuawa watu 18 wengi wao wakiwa ni askari wa Imarati katika shambulizi la kombora lililoilenga kambi ya kijeshi ya askari hao katika eneo la al-Bariqai katika mkoa huo wa Aden. Hii si mara ya kwanza kwa askari wa kigeni wanaoshirikiana na Saudia katika vita vya kichokozi nchini Yemen kuuawa na wanamapambano wa taifa hilo.
chanzo-tehranradio
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :