technology

Marekani yalaumu Afghanistan kwa shambulio Kunduz,Raia Syria wadhihirisha mapenzi yao kwa Rais Putin,Bale atisha kwa ubora nchi wales



MSF

Jenerali mmoja mkuu wa jeshi la Marekani amesema wanajeshi wa Afghanistan ndio walioomba majeshi ya taifa hilo yashambulie kliniki iliyokuwa ikitumiwa na shirika la madaktari wasio na mipaka la Medecins Sans Frontieres (MSF) mjini Kunduz.
Jenerali John Campbell alikiri kuwa wanajeshi wa Marekani hawakuwa wameshambuliwa kufikia wakati huo.
MSF imesema juhudi za Afghanistan kutana kuonyesha shambulio hilo lilikuwa la haki ni “kukiri kosa la uhalifu wa kivita”.
Wanajeshi wa Afghanistan wakisaidiwa na wenzao wa Marekani wamefanikiwa kukomboa maeneo mengi ya Kunduz, mji uliokuwa umetekwa na wapiganaji wa Taliban wiki iliyopita.
Wafanyakazi 12 wa MSF na wagonjwa 10 walifariki kwenye shambulio hilo lililotekelezwa na Marekani.
Shirika la MSF linasema hospitali hiyo ilikuwa ikitegemewa sana na maelfu ya wakazi wa jiji hilo na maeneo mengine ya Afghanistan kaskazini.
"Tumefahamu sasa kwamba mnamo Oktoba 3, wanajeshi wa Afghanistan walisema walikuwa wakishambuliwa na adui na wakaomba usaidizi wa angani kutoka kwa wanajeshi wa Marekani,” alisema Jenerali Campbell, ambaye ni kamanda mkuu wa majeshi ya shirika la kujihami la Nato yanayoongozwa na Marekani ambayo yanahudumu Afghanistan.
“Shambulio la kutoka angani lilihitajika kuangamiza hatari ya Taliban na raia walishambuliwa kimakosa,” alisema.
Aliomba radhi kutokana na vifo hivyo vya raia.
Akijibu matamshi hayo ya Jenerali Campbell, mkurugenzi mkuu wa MSF Christopher Stokes, ameituhumu Marekani kwa “kujaribu kupitisha lawama kwa serikali ya Afghanistan”.
“Ukweli ni kwamba Marekani ndio walioangusha mabomu hayo,” Bw Stokes alisema.
“Marekani walishambulia hospitali kubwa iliyojaa majeruhi na wafanyakazi wa MSF.”
#HABARI 2#######
Raia Syria wadhihirisha mapenzi yao kwa Rais PutinRaia wa Syria wamedhihirisha imani na mapenzi yao kwa Rais Vladmir Putin wa Russia kutokana na hatua yake ya kuendesha mashambulizi ya anga dhidi ya magenge ya kigaidi nchini mwao. Wakazi wa miji ya Tartus, Lattakia na miji mingine ya Syria wamekaribisha hatua ya jeshi la Russia kuanzisha hujuma dhidi ya magaidi nchini mwao na kusema kuwa, wanataraji kwamba mashambulio hayo yatakuwa sababu ya kuangamizwa genge la kitakfiri la Daesh. Raia hao wa Syria ambao wamemtaja Rais Putin kwa jina la 'Mshindi na mwokozi wao mbele ya Madaesh' ambao wamechafua eneo zima la Mashariki ya Kati, wanaamini kuwa operesheni ya Russia dhidi ya genge hilo la kigaidi yatamaliza machafuko nchini mwao ambayo yamedumu kwa miaka kadhaa sasa. Aidha raia hao wa Syria wameituhumu Marekani na waitifaki wake ikiwemo Uturuki, Saudia, Qatar na baadhi ya nchi kwa kuyaunga mkono kifedha na kisilaha kwa makundi ya kigaidi na kitakfiri kama vile Daesh, Jab'hatu Nusra na mengineyo, yanayofanya jinai na mauaji ya kutisha  dhidi yao. Wamesema kuwa, kitendo cha Marekani na nchi hizo kuchukizwa na mashambulizi ya anga ya Russia dhidi ya magenge hayo, kinadhihirisha ni kwa namna gani Washington ilivyo mstari wa mbele katika kuwaua Wasyria kupitia magaidi hao maarufu kwa kutenda jinai.
#mchezo#######
mshambuliaji wa pembeni katika klabu ya Real madrid nchini Hispania GARETH BALE usiku wa kuamkia leo alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka kupitia chama cha soka nchini wales(FAW),Bale ametangazwa kuwa mchezaji bora hapo jana ikiwa ni mara yake ya tano kuchukua nafasi hiyo.
BALE pia ametangazwa kuwa mchezaji bora wa tuzo ya mashabiki ,ambayo tuzo hiyo inaambatana na tuzo ya ya chama cha soka nchini humo (FAW).


Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :