watu 4 wanusurika kufa maji TANGA
Watu wanne wanusurika kufa maji wilayani PANGANI mkoani TANGA baada ya chombo chao aina yangalawa kuzama baharini kufuatia mvua na hali mbaya ya hewa.
watu hao waliozama juzi wameokotwa jana katika kisiwa cha ZANZIBAR huko nungwi na chombo chao kuokotwa katika kisiwa cha MAZIWE kilichopo Wilayani PANGANI mkoani TANGA.
Na kwamuji wa ndugu wa wavuvi hao wamesema ndugu zao wameokolewa na kwa sasa wako salama lakini bado wako huko visiwani ZANZIBAR.
Lakini Hali mbaya ya hewa bado imekua ikiyaandama maeneo mengi ya ukanda wa BAHARI ya HINDI hususani PANGANI,ambapomvua na upepo mkali umekua ukivuma mara kwa mara.
TANZANIA imetangaza masiku kadhaa yalio pita kuwa kutakua na mvua kubwa za mvululizo kuanzia mwezi wa tisa na imetoa tahadhari kwa wale wote wanaokaa mabondeni kuhama katika maeneo hao.
Labels
MIKOANI
Post A Comment
Hakuna maoni :