NIMEKUSOGEZEA HII MTU WANGU!!!!!!!Lil Wayne na Christina Millian waachana..!? Sababu? Ninayo yote hapa…

Baada ya kuachana na mchumba wake miaka miwili iliyopita mwimbaji wa R&B Christina Millian alianza kuonekana sana na rapper Lil Wayne baada
ya kujiunga na lebo ya msanii huyo, muda mfupi badaae wawili hao
wakaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na mpaka sasa wana zaidi ya
mwaka mmoja pamoja.
Lakini leo headlines za wawili hawa ni
tofauti kidogo… wapenzi hao wamethibitisha kuwa wameachana toka mwezi
uliyopita lakni waliamua kukaa kimya kwanza na kuweka baadhi ya mambo
yao sawa kabla kutangaza kwa watu kuwa uhusiano wao wa kimapenzi
umeisha.

Msemaji wa karibu wa watu hao anasema sababu kubwa iliyopelekea kuachana kwao zinatokana na ratiba za wawili hao kubana sana.
>>>“Wanaachana
sio kwamba wanapenda ila ratiba zao zinawabana sana, wanakosa muda wa
kuonana na kuwa pamoja, Lil Wayne anafanya sana tour za wasanii wake na
za kwake pia na pia anaifanyia kazi album ya Christina Millian…
isitoshe hata Christina Millian ana mambo meng, vipindi vya TV, Talk
Shows za kuandaa na vingine vingi, so wameona bora waachane lakini sio
kwa sababu wamechokana ila ratiba za kazi haziwapi muda wa kuwa pamoja”. <<< Alisema msemaji wa karibu wa mastaa hao.
chanzo- http://millardayo.com
chanzo- http://millardayo.com
Labels
burudani
Post A Comment
Hakuna maoni :