HABARIKA NA HIII!!!! Dada Dj mkenya ashinda tuzo la Nollywood

Mwanadada Dj kutoka
nchini Kenya Pierra Makena ametunikiwa tuzo kama mcheza filamu bora kwa
kushiriki katika filamu moja ya kinigeria ya "When Love Comes Around,"
wakati wa awamu ya tano ya tuzo za Nollywood ambazo pia zinafahamika kwa
tuzo za Oscar za Afrika.
Dj huyo anayeendesha mambo yake kwenye
mji mkuu wa Kenya Nairobi, anasema alishangazwa na tuzo hilo licha ya
yeye kuwa maarufu katika nyanja ya muziki tu.
Makena alielezea furaha yake baada ya ushindi huo na kuandika kwenyr mtandao wa Instagram akisema kuwa, Mabibi na Mabwana, Nimeshinda! Nimeshinda! Nimeshinda!
chanzo bbc swahili.com
Labels
burudani
Post A Comment
Hakuna maoni :