Baada ya dili lakwenda Madrid kukwama, De Gea amethibitisha kufanya uamuzi huu…

Takribani siku 10 tangu uhamisho wake wa kwenda kujiunga na klabu ya Real Madrid kukwama, golikipa wa timu ya taifa ya Spain na klabu ya Manchester United, David De Gea ameamua kufanya uamuzi mwingine kuhusu hatma yake ndani ya klabu hiyo ya Uingereza.

David de Gea amesaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Manchester kwa miaka mengine minne baada ya mkataba wake wa sasa kuisha mwakani.
Golikipa huyo mwenye miaka 24 alianza
mazungumzo ya mkataba mpya baada ya uhamisho wake ambao ungegharimu
kiasi cha Pound Mil. 29 kushindikana siku ya mwisho ya dirisha la
usajili.
Hii ni #Tweet ya De Gea akitghibitisha kubakia Man United.

Mkataba mpya wa De Gea utamfanya kuwa golikipa anayelipwa zaidi kwa kulipwa mshahara usiopungua kiasi cha Pound laki mbili kwa wiki.
chanzo- http://millardayo.com
Labels
MICHEZO
Post A Comment
Hakuna maoni :