Shambulio la Syria laua watu kumi

Hata hivyo vikosi cha kikurdi vimejipanga kukabiliana na wanamgambo wa dola ya kiislamu , ambacho mara nyingi hufanya mashambulizi ya aina hiyo.
Wakati huo huo,umoja wa mataifa umesema Syria linakabiliwa na homa ya matumbo katika kambi ya wakimbizi ya Yarmouk ambayo ipo kwenye vitongoji vya Syria ndani ya mji mkuu wa Damascus.
Msemaji wa umoja wa mataifa amesema kuwa ugonjwa huo umshamiri katika kambi hiyo ya wakimbizi yapata miezi sita sasa.inaelezwa kuwa Yarmourk ni eneo ambalo linakumbwa na majanga kila mara .
Ingawa eneo hilo liko chini ya himaya ya serikali tangu mwaka 2013 lakini bado hali imezidi kuwa tete tangu kikosi cha wanamgambo wa dola ya kiislamu IS walipowavamia katika kambi hiyo na kuangamiza watu.
(chanzo bbcswahili.com)
Post A Comment
Hakuna maoni :