Ombi la kuishtaki Kenya ICC lakataliwa
Mahakama
ya rufaa ya kimataifa ya jinai, ICC, iliyoko Hague, Uholanzi
imetupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na mwendesha mashtaka mkuu wa
mahakama hiyo Fatouh Bensouda, ya kutaka mahakama hiyo kuishtaki Kenya
katika kongamano la kimataifa ya nchi wanachama wa mahakama hiyo.
Bensouda
aliitaka mahakama hiyo kuizomea serikali ya Kenya kuwa imekataa
kushirikiana na mahakama hiyo wakati ilipokuwa ikikusanya ushahidi dhidi
ya rais Uhuru Kenyatta.Aidha Bensouda aliliambia mahakama hiyo kuwa Kenya ilificha ushahidi ambao ungetumika dhidi ya rais Kenyatta.

Lakini majaji waliokuwa wakisikiliza rufaa hiyo wamesema kuwa mahakama ya chini ya ICC, ilifanya kosa kuwasilisha kesi hiyo kwa mahakama ya rufaa.
Majaji hao walisema mahakama iliyokuwa ikisikiliza kesi dhidi ya Kenya, haikuchunguza vyema maombi yaliyowasilishwa na mwendesha mashtaka, na hivyo kufanya kosa kuwasilisha keshi hiyo kwa mahakama ya rufaa.
Aidha majaji hao wamesema kuwa mahakama hiyo haihoji ikiwa masuala yote ya kisheria yalikuwa yametumika kabla ya kuamua ikiwa kenya itawasilishwa mbele ya baraza la nchi wanachama.

Majaji hao wa mahakama ya rufaa walisema wao hawana mamlaka ya kuamua kuishtaki Kenya mbele ya baraza hilo na kuwa uamuzi wa mahakama ya chini ulikuwa na dosari.
Bensouda alikuwa amewasilisha kesi kuitaka hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya Kenya kwa kukosa kushirikiana vyema na maafisa wa mahakama hiyo, wakati ilipokuwa ikijaribu kukusanya ushahidi dhidi ya rais Uhuru Kenyatta, madai ambayo yalipingwa vikali na Kenya.

Lakini machi mwaka huu mahakama hiyo iliamua kufutilia mbali mashtaka yote dhidi ya rais Kenyatta baada ya mwendesha mashtaka kufahamisha mahakama hiyo kuwa hakuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo, kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha, na kuwa baadhi ya mashahidi wake walikuwa wameamua kutoshirikiana na mahakama hiyo.
Kesi hiyo dhidi ya Kenya sasa itasikilizwa upya na mahakama ya chini
(chanzobbcswahili.com)
Post A Comment
Hakuna maoni :