Mamia wahofiwa kufa maji katika pwani ya Libya

Maafisa wa Libya wanasema boti ya kwanza ambayo iliomba msaada mapema ilikuwa na wahajiri 50 na nyingine ambayo ilizama baadaye ilikuwa na wahamiaji zaidi ya 400.
Karibu watu 201 wameokolewa na askari wa pwani wa Libya lakini mamia ya wengine wanahofiwa kuwa wamekufa maji.
Wakazi wa mji wa Zuwara huko kaskazini magharibi mwa Libya wanasema maiti za watu wasiopungua 100 zimewasilishwa katika hospitali ya mji huo. Wahanga hao ni wahajiri kutoka nchi za Syria, Bangladesh na nchi kadhaa za Kiafrika za kusini mwa jangwa la Sahara.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa wahajiri wapatao 2400 wamefariki dunia mwaka huu wakijaribu kuvuka Bahari ya Mediterranean kuelekea Ulaya.
(tehran ihaa ya kiswahili)
Post A Comment
Hakuna maoni :