HRW: Saudia imetumia silaha za kemikali Yemen

Human Rights Watch pia limetaka kuundwe tume ya kimataifa ya kuchunguza ukiukaji wa sheria za kimataifa za vita unaofanywa na Saudi Arabia nchini Yemen.
Taarifa ya HRW imesema Saudia imetumia mabomu ya vishada katika mashambulizi yasiyopungua saba kwenye mkoa wa Hajja huko kaskazini mwa Yemen pekee ambayo yameua raia wengi. Taarifa hiyo imewataka watawala wa Riyadh kukomesha utumiaji wa silaha hizo haraka iwezekanavyo. Imesema mashambulizi hayo ya mabomu ya vishada yalilenga ovyo makazi ya raia wa Yemen. Human Rights Watch imelitaka Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuunda tume ya kuchunguza jinai hizo za Saudia.
Mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu shirika la Human Rights Watch lilisema kuna ushahidi kuwa Saudia imetumia mabomu yaliyopigwa marufuku katika mashambulizi yake za angani dhidi ya maeneo ya raia nchini Yemen. Mabomu hayo ya vishada yametengenezwa nchini Marekani.
(chanzo tehran idhaa ya kiswahili)
Post A Comment
Hakuna maoni :