technology

Waziri wa Ndani wa Kenya aitaka CNN kuomba radhi

Waziri wa Ndani wa Kenya aitaka CNN kuomba radhiWaziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya ameitaka kanali ya televisheni ya CNN ya Marekani kuwaomba radhi Wakenya kwa kuitaja nchi hiyo kuwa ni uwanja wa ugaidi.
Joseph Nkaissery amesema: Kama televisheni ya CNN imestaarabika vya kutosha basi ilipaswa kuwaomba radhi Wakenya. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya amesema nchi hiyo inakabiliwa na mashambulizi ya kigaidi kama zilivyo nchi nyingine dunia lakini suala hilo haliifanyi kuwa eneo salama kwa ugaidi. Waziri Mkaisserry amewataka Wakenya kuidharau ripoti ya televisheni ya CNN kama inavyostahiki.
Msimamo huo mkali wa Kenya umekuja baada ya kituo cha televisheni ya CNN cha Marekani kupeperusha habari iliyodai kuwa Kenya ni 'uwanja wa ugaidi', siku moja kabla ya Rais wa Marekani kuwasili nchini humo. CNN ilipeperusha habari iliyodai, "Rais Barack Obama sio tu anaenda nyumbani kwa babake, pia anazuru 'uwanja wa ugaidi."
Rais Barack Obama wa Marekani anatarajiwa kuwasili leo Ijumaa nchini Kenya kwa ziara ya siku tatu

(chanzotehran idhaa radio)
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :