
Kwa uchache raia 19 wa Yemen wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa
katika mashambulio mapya ya anga ya Saudia katika maeneo mbalimbali ya
nchi hiyo. Ripoti kutoka nchini Yemen zinasema kuwa, watu 6 wa familia
moja wameuawa baada ya ndege za kijeshi za Saudia kufanya mashambulio
katika nyumba moja kaskazini magharibi mwa jimbo la Sa'ada. Taarifa
zaidi zinasema kuwa, tangu asubuhi ya leo mji wa Sa'ada kwa uchache
umeshambuliwa mara 21. Raia wengine wa Yemen wameuawa leo katika mji wa
Hajjah kufuatia mashambulio mengine ya anga ya Saudia. Mashambulio ya
kinyama ya Saudia nchini Yemen yameendelea kusababisha mauaji kwa raia
wasio na hatia na uharibifu mkubwa kwa nchi hiyo ambayo kwa sasa
inakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu.
Hadi sasa watu wasiopungua 3000 wameuawa tangu Riyadh ilipoivamia na
kuanza kufanya mashambulizi ya kinyama dhidi ya Yemen tarehe 26 Machi
mwaka huu. Mashirika ya misaada ya kibinadamu yameendelea kutoa
tahadhari kuhusiana na hali mbaya ya kibinadamu inayoikabili nchi hiyo.
(chanzo tehran idhaa ya kiswahili)
http://kiswahili.irib.ir/habari/uadui/item/50164-raia-19-wa-yemen-wauawa-katika-mashambulio-ya-saudia
Post A Comment
Hakuna maoni :