technology

Obama aikabidhi Kongres mapatano ya nyuklia ya Iran

Obama aikabidhi Kongres mapatano ya nyuklia ya  IranSerikali ya Marekani imewasilisha rasmi kwa bunge la Congress mapendekezo ya nyuklia yaliyofikiwa wiki iliyopita kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi za kundi la 5+1 na kutoa wito kwa bunge hilo kuidhinisha makubaliano hayo. Congress itakuwa na siku 60 za kupitia na kupigia kura makubaliano ya Vienna ingawa Rais Obama ametangaza wazi kwamba atapiga veto maamuzi yoyote ya bunge hilo yatakayolenga kukwamisha utekelezaji huo.
Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel ameitaka Congress ya Marekani kuyakataa makubaliano hayo. Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry amemjibu Netanyahu kwa njia isiyo ya moja kwa moja akisema wanaopinga makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na 5+1 wanaishi katika ulimwengu wa ndoto.
Huku hayo yakijiri na katika kile kinachoonekana kama hatua za awali za nchi za Ulaya kujipanga kurudisha uwekezaji hapa Iran, Waziri wa Uchumi wa Ujerumani, Sigmar Gabriel, amewasili mjini Tehran akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa wanabiashara ambapo anatarajiwa kukutana na viongozi mbalimbali na wanabiashara wakubwa nchini hapa.

(chanzo tehran radio)
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :