
Seneta John McCain wa jimbo la Arizona nchini Marekani ameikosoa vikali
serikali ya Rais Barack Obama wa nchi hiyo kwa kushindwa kukabiliana na
kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh. McCain amesema kuwa mashambulio
ya ndege za kivita za Marekani dhidi ya kundi hilo hayajakuwa na athari
yoyote ya maana katika kudhoofisha na kulitokomeza kundi hilo
linaloendelea kufanya uharibifu na mauaji makubwa katika nchi za
Kiislamu. Ameongeza kuwa licha ya kuwa Marekani inadhibiti anga ya
maeneo yanayoshikiliwa na kundi hilo la kitakfiri na Kizayuni, lakini
kundi hilo linaendelea kukwepa mashambulio hayo ya Marekani na kudumisha
shughuli zake za kuwasajili wanachama zaidi kupitia mitandao ya kijamii
kwa kujificha katika maeneo ya mijini.
McCain amesema Marekani
inapasa kuongeza juhudi zake za kuyaelimisha makabila ya Kisuni na
askari usalama wa Iraq pamoja na wapinzani wa Syria ili eti kupata
matokeo ya kuridhisha katika mapambano yake dhidi ya Daesh. Akizungumza
hapo jana Jumatatu, Rais Obama alisema kuwa Washington kwa sasa haina
mpango wowote wa kutuma askari zaidi nje ya nchi na kwamba inakusudia
kuharakisha mwenendo wa kuipa Iraq silaha za kulenga vifaru.
Post A Comment
Hakuna maoni :