technology

Idadi ya Wamarekani wanaokana uraia yaongezeka

Raia 1,426 wa Marekani wameukana uraia wao katika kipindi cha miezi mitatu ya tatu ya mwaka huu wa 2015.
Televisheni ya Press TV imeinukuu Wizara ya Hazina ya Marekani ikitangaza kuwa, idadi ya wananchi wa nchi hiyo wanaoukana uraia wao imeshafikia 3,221 mwaka huu.
Mwaka 2014 wananchi 3,415 wa Marekani waliukana uraia wao na kurejesha pasi zao za kusafiria kutokana na kodi kubwa wanayotozwa nchini humo.
Idadi hiyo imeongezeka mno kiasi kwamba, mwaka 2008, wananchi 231 tu wa Marekani ndio walioukana uraia wao.
Raia wengi wa Marekani wanalalamikia dhulma na kuongezeka ukosefu wa uadilifu katika jamii ya nchi hiyo kwenye miongo ya hivi karibuni.
Katika miaka ya baina ya 1968 na 2006 raia wa Marekani waliokuwa na imani na nchi yao ilipungua kutoka asilimia 56 hadi 34.
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :