technology

Watu kadhaa wauawa kwenye mapigano Kongo DR

Watu kadhaa wauawa kwenye mapigano Kongo DR Duru rasmi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana ziliripoti habari ya kuuawa watu kadhaa katika mapigano na ghasia mashariki mwa nchi hiyo. Duru ya usalama katika mkoa ulioathiriwa na machafuko wa Kivu ya Kaskazini mashariki mwa Kongo imetangaza kuwa watu wasiopungua watatu wameuawa kwenye mapigano hayo na makumi ya wengine kujeruhiwa na kwamba uchunguzi umeanzishwa ili kuwasaka wahusika wa mauaji hayo. Itakumbukwa kuwa watu watano waliuliwa na wengine 22 kujeruhiwa katika mapigano yaliyotokea tarehe 24 Aprili mwaka huu katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini. Mauaji hayo yanajiri mkoani humo huku hali ya usalama ikizidi kuzorota huko Kivu ya Kaskazini. Wiki iliyopita pia wanajeshi wawili wa kulinda amani na raia wawili waliuawa katika mkoa huo katika shambulizi la kuvizia la waasi wa Uganda.
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :