technology

Wapalestina wazuiwa kuinga Jerusalem

Image copyrightAFP
Image captionWapalestina wazuiwa kuinga Jerusalem
Polisi wa Israeli wametangaza marufuku ya kuingia kwenye mji wa kale wa Jerusalem hatua ambayo itasababisa wapalestina kutoruhusiwa eneo hilo kwa siku mbili.
Hii ni baada ya mashambulizi yaliyofanyika dhidi ya raia wa Israeli siku ya Jumamosi na Jumapili asubuhi.
Wawili hao waliuawa kwa kuchomwa kisu na mpalestina, huku kijana mmoja naye akijeruhiwa katika kisa tofauti.
Image copyrightAFP
Image captionWaziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu anafanya mkutano wa dharura na baraza la mawaziri
Polisi waliwaua kwa kuwapiga risasi washambuliaji hao.
Wapalestina hawaruhusiwi kuingia eneo hilo isipokuwa wale wanaoishi huko.
Hata hivyo waisraeli na wamiliki wa biashara pamoja na wanafunzi pekee ndio watakaoruhusiwa kuingia.
Image copyrightEPA
Image captionUtawala wa Palestina umekashifu hatua ya Israeli ya kupalia cheche za uhasama
Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu anafanya mkutano wa dharura na baraza la mawaziri kujadili matukio hayo.
Utawala wa Palestina umekashifu hatua ya Israeli ya kupalia cheche za uhasama katika ukingo wa Magharibi na Jerusalem katika kipindi cha hivi punde.
chanzo-bbcswahili.com
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :