Watu zaidi ya 114,000 wameikimbia nchi ya Kiarabu ya Yemen kutokana na vita na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi watu laki mbili ifikapo mwishoni mwa mwaka kesho.
Mapigano yalishika kasi Yemen mwezi Machi mwaka huu wakati yalipoanza mashambulizi ya kijeshi yaliyoongozwa na Saudia dhidi ya wapiganaji wa Kihuthi ili kumrejesha madarakani Rais Abdul Rabu Mansour Hadi wa nchi hiyo. Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) na Taasisi ya Kimataifa ya Uhamiaji (IOM) zimesema kuwa Wayemeni wasiopungua elfu sabini wamewasili Djibouti, Ethiopia na Sudan.
Wayemeni wengine 44,080 wamekimbilia Saudi Arabia na Oman. Taasisi ya IOM imesema kuwa idadi ya watu waliokimbia Yemen na
kuelekea katika nchi jirani inatazamiwa kuongezeka na kuwa zaidi ya laki mbili hadi kufikia mwishoni mwa mwaka ujao. Wakati huo huo Umoja wa
Mataifa umesema kuwa vita vya Yemen hadi sasa vimeuwa watu wasiopungua elfu tano na kujeruhi wengine 25,000, wengi wakiwa ni raia
wa kawaida.
chanzo-tehran radio
Post A Comment
Hakuna maoni :