Polisi nchini Pakistan wanasema kuwa
watu wenye silaha wamemuua kwa kumpiga risasi mwandish maarufu wa
habari katika mji wa Karachi.
Shambulizi hilo kwa mujibu wa idara ya polisi ni la tatu dhidi ya waandishi habari katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
Aftab Alam alikuwa ni mwandishi wa habari wa eneo la kusini mwa Pakistan wa runinga ya kibinafsi ya Geo News.
Nia ya shambulizi hilo haijabainika hadi sasa. Image copyrightAFP
Watu wenye silaha wamemuua kwa kumpiga risasi mwandishi maarufu wa habari katika mji wa Karachi.
Jana usiku mtu aliyekuwa amejihami kwa bunduki alimpiga risasi na kuua fundi mitambo wa runinga hiyo hiyo ya Geo.
Dereva wa gari la kampuni hiyo anauguza majeraha.
Huko Peshawar mwandishi wa habari wa runinga ya taifa alipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya.
NI MWANDISHI WA TOP NEWS BLOG, AMESHAFANYA KAZI YA UANDISHI NA UTANGAZAJI KATIKA KITUO CHA RADIO-PANGANI FM RADIO,LAKINI KWA SASA ANAENDELEA NA ELIMU YA JOURNALISM KATIKA NGAZI YA DIPLOMA-MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO-TANZANIA
Post A Comment
Hakuna maoni :