JE!!wajua!!!!!Matokeo kinyume yanayotokana na siasa hasi za Saudi Arabia
Mwenendo wa siasa hasi za Saudi Arabia yakiwemo mashambulizi yake
ya kichokozi nchini Yemen na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la
dunia, ni mambo yaliyoiletea nchi hiyo matokeo yaliyo kinyume na
matarajio yake ya awali. Shirika la ndege la Saudia limetangaza kuwa,
kutokana na mashambulizi ya jeshi la Yemen na wapiganaji wa kujitolea wa
taifa hilo katika maeneo ya mpakani, safari za ndani na nje katika
viwanja vya ndege vya miji ya Jazan, Abha, Wadi Aldwasir, Bishah,
Sharorah na Najran, hadi zimesimamishwa hadi pale litakapotolewa tangazo
jipya baadaye. Tangu Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud aingie
madarakani nchini Saudia, siasa za nje za nchi hiyo zimegeuka na kuwa za
uvamizi na mashambulizi. Siasa za uvamizi za utawala wa Aal-Saud
zilianzia huko Yemen hapo tarehe 26 mwezi Machi mwaka huu. Watawala wa
Riyadh walidhani kwamba, vita dhidi ya Yemen vingemalizika ndani ya muda
mfupi sana, hata hivyo miezi mitano na nusu imepita sasa ambapo si tu
kwamba Saudia imeshindwa kufikia hata mafanikio madogo katika vita
hivyo, bali pia mgogoro wenyewe wa Yemen umehatarisha usalama wa utawala
wa Aal-Saud. Katika mbadiliko mapya kabisa, wapiganaji wa Harakati ya
Kiislamu ya Answarullah na jeshi la Yemen, wamevurumisha makombora
kadhaa katika maeneo ya mpakani ya Saudia na hivyo kulitia hasara kubwa
jeshi la nchi hiyo. Gadi ya ikulu ya rais wa Yemen pia imetangaza kuwa,
ikiwa mashambulizi ya Saudia yataendelea, basi haitasita kutumia
makombora yake ya masafa marefu kuishambulia miji kadhaa ya Saudia,
ukiwamo mji mkuu wa nchi hiyo Riyadh. Katika radiamali juu ya tishio
hilo la viongozi wa Yemen, serikali ya Riyadh, imeamua kufunga viwanja
vyake vya ndege katika miji ya kusini mwa nchi kwa kuhofia kushambuliwa
na makombora hayo ya masafa marefu. Kwa msingi huo tunaweza kusema kuwa,
vita vya Saudi Arabia dhidi ya taifa la Yemen, kinyume na malengo ya
kuinua nafasi ya watawala wa nchi hiyo, vimesababisha uharibifu mkubwa
na mauaji ndani na nje ya nchi hiyo, na wakati huohuo kudhoofika nafasi
ya mfalme huyo pamoja na mwanaye, katika fikra za raia wa Saudia na hata
katika eneo. Kutokana na hasara kubwa iliyowasababishia raia wa Yemen,
Riyadh imefananishwa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, kiasi cha
Mfalme Salman kudharauliwa katika fikra za walio wengi duniani na
kutajwa kuwa jenerali mtoto. Kwa hakika hilo sio suala pekee
lililouletea natija kinyume utawala wa Aal-Saud. Hatua ya utawala huo ya
kushusha bei ya mafuta kwa lengo la kutoa mashanikizo kwenye uchumi wa
Iran na Russia, imekuwa na natija kinyume ambapo imegeuka na kuwa kwa
madhara ya utawala wa Riyadh. Katika ripoti ya hivi karibuni kabisa,
Waziri wa Mafuta wa Saudia ametangaza kuwa, madhara yanayotokana na
kushuka bei ya mafuta katika soko la dunia, yameifanya nchi hiyo
kukabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi. Ukweli ni kwamba, ili Saudia
iweze kujionyesha kuwa taifa lenye nguvu katika eneo la Mashariki ya
Kati, inahitajia kwanza kupata viongozi wenye tajriba ambao katika
maamuzi yao ya siasa za kigeni, watafuata mkondo wa akili na fikra
salama, kinyume na kutumia mabavu na mauaji.
(chanzo-tehranradio)
(chanzo-tehranradio)
Post A Comment
Hakuna maoni :