HALI MBAYA YA USAFI WA FUKWE TANGA
Wananchi wa kijiji cha
kipumbwi wilayani pangani wametakiwa kutotupa taka katika fukwe za bahari ya
hindi na kushiriki katika kusafisha mazingira ya bahari kwa ujumla.
Akiongea na TOP NEWS BLOG katibu wa BMU MUSA OMARI MASUDI kijiji cha kipumbwi, katika mkutano ulio
itishwa na shirika lisilo la kiserikali la SEA SENSE, ametoa wito kwa wananchi
wa kipumbwi kuacha tabia hiyo kwani inasababisha mripuko wa magonjwa,na
kupelekea vifo kwa viumbe walioko baharini.
Na kwaupande wake mwenyekiti
wa kitongoji HASANI MUHAMMEDI amewataka wakazi wa kipumbwi kuona umuhimu wa
kusafisha mazingira ya BAHARI na FUKWE na suala la kusafisha ufukwe na la watu
wote na sio BMU peke yao.
Hayo yamejiri jana
katika mkutano uliotishwa na shirika la SEA SENSE linalo toa elimu juu ya
uhifadhi wa mazingira BAHARI, FUKWE na kupiga
vita uvuvi haramu katika WILAYA ya PANGANI
Labels
MIKOANI
Post A Comment
Hakuna maoni :