
Klabu ya Southampton ya Uingereza
imakubali kuwa Manchester United wanavutiwa na wana mpango wa kumsajili
winga kutoka nchini Senegal Sadio Mane. Ieleweke kwamba, United ilifanya
jitihada kumapata mchezaji huyo mwenye miaka 23 tokea juma lililopita
lakini Southampton wamekanusha kupokea ofa yoyote.
Mshambuliaji wa
Barcelona Pedro amekuwa akihisiwa kujiunga na United lakini kwa sasa
yupo katika hatua za mwisho za kijiunga na Chelsea kwa dau la pauni
milioni 21.
Mane alifunga magoli 10 katika michezo 32 aliyocheza
msimu uliopita baada ya kujiunga na klabu yake ya sasa akitokea Red Bull
Salzburg ya Austria na yumo pia katika orodha ya wachezaji waliowahi
kufunga magoli matatu (hat-trick) kwa muda mfupi zaidi.
(chanzo bbcswaili.com)
Post A Comment
Hakuna maoni :