Milipuko kadhaa yatikisa jiji la Cairo
Vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali ya Misri vimetangaza kuwa milipuko hiyo mitatu imetokea katika wilaya ya Shubra al-Khaima. Wizara ya Afya ya Misri imetangaza kuwa watu 22 wamejeruhiwa katika milipuko hiyo ingawa vyombo vya habari vya kujitegemea vimesema ni mapema kuweza kujua idadi ya watu waliouawa au kujeruhiwa katika milipuko hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo.
Misri imekuwa ikilengwa kwa mashambulizi yanayofanywa na wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh ambayo kwa kawaida yanalenga taasisi za serikali hususan ofisi na idara za polisi na askari usalama
\(chanzo tehran radio idhaa ya kiswahili)
Post A Comment
Hakuna maoni :