technology

Majeshi ya Korea Kaskazini yajiandaa kuingia vitani

Majeshi ya Korea Kaskazini yajiandaa kuingia vitani Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amevitaka vikosi vya mpakani vya nchi hiyo kujiweka katika mazingira ya kuingia vitani wakati wowote. Kiongozi wa Korea Kaskazini ametoa amri hiyo baada ya kushadidi hitilafu na mivutano kati ya nchi yake na jirani yake Korea Kusini. Kim Jong-un aidha ametoa amri hiyo ambayo inaanza kutekelezwa leo baada ya pande mbili kushambuliana kwa mizinga katika maeneo wa mpaka wa nchi mbili hizo yenye ulinzi mkali. Kiongozi wa Korea Kaskazini ameyataka majeshi ya nchi yake yaliyoko mpaka kujiweka tayari kabisa na kujizatiti kwa silaha kwa ajili ya vita itakapofika saa 11 jioni leo kwa majira ya nchi hiyo.
Korea Kusini nayo imeviweka tayari vikosi vyake vya kijeshi baada ya muda ulioainishwa na Pyongyang kwa Seoul ya kuondoa vipaza sauti vyake vya matangazo katika maeneo ya mpakani. Jana Korea Kaskazini  iliipatia Korea Kusini masaa 48 iwe imezima vipaza sauti vyake vya matangazo na kwamba, itakabaliwa na shambulio la kijeshi endapo haitafanya hivyo baada ya muda ulioainishwa kumalizika.

(chanzo tehrani radio)
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :