technology

Burundi matatani baada ya mwanasiasa kuuawa

Burundi matatani baada ya mwanasiasa kuuawaMauaji yaliyotokea jana dhidi ya kiongozi mwingine wa chama cha upinzani nchini Burundi yamezidisha hali ya wasiwasi na mgororo wa ndani ya nchi hiyo.
Pontien Barutwanayo ambaye ni mwanachama mwandamizi wa chama kikuu cha upinzani cha National Liberation Forces (FNL) alipigwa risasi na kuuawa jana akiwa katika baa moja katika eneo la Isale umbali wa kilomita 18 kutoka Bujumbura. Watu wengine watatu walijeruhiwa katika shambulizi hilo. Chama cha FNL kilisusia chaguzi za Rais na Bunge zilizofanyika mwezi Julai mwaka huu. Mauaji hayo ya Barutwanayo ndiyo ya hivi karibuni kufanywa nchini Burundi katika machafuko ya kisiasa kati ya kambi ya upinzani na chama tawala cha Rais Pierre Nkurunziza.
Burundi ilitumbukia katika ghasia na machafuko baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kugombea tena kiti hicho kwa mara ya tatu mfululizo, suala ambalo limepingwa na kambi ya upinzani iliyosema ni ukiukaji wa sheria na katiba ya nchi hiyo
(chanzo tehran radio idhaa ya kiswahili)
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :