Wakati Afrika ikipambana na janga la kupungua kwa TEMBO Zimbabwe yauza Tembo wake China
Wahifadhi wanyama wanasema tembo wanahitaji uangalifu wa miaka kadhaa kutoka kwa wazazi wake na kwahivyo kuwatenganisha tembo hao wadogo kutoka jamii zao katika umri mdogo ni kitendo cha ukatili na kitakacho kuwa na athari kubwa kwa wanyama hao.
Tembo hao wataishi katika mbuga ya wanyama karibu na mji uliopo kusini - Guangzhou. Inasemekana kwamba wanyama katika mbuga hiyo wanateswa na kuwekwa katika mzingira mabaya.
Raia wengi wa Zimbabwe wanaona tembo kama wanyama waharibifu wanaoharibu mazao na kuangusha miti.
Chanzo (bbcswahili.com)
Post A Comment
Hakuna maoni :