technology

UN yasisitiza kufuatwa misingi ya Mandela

Image result for mandelaMjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesisitiza kuwa, Nelson Mandela ameufanya ulimwengu kuwa eneo bora la kuishi. Akizungumza jana Jumamosi kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Martin Kobler  amesema kuwa Mandela ameifanya dunia kuwa mahala bora pa kuishi, na kwamba Mandela anaendelea kuwa shakhsia wa kuigwa na watu wote. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameongeza kuwa: Kutatuliwa mizozo na mivutano, kuuunga mkono haki za binadamu, kupambana na ubaguzi wa rangi na kijinsia na kuanzisha umoja wa kitaifa, yote hayo yanawezekana iwapo misingi ya Mandela itafuatwa. Nelson Mandela Rais wa zamani wa Afrika Kusini alizaliwa tarehe 18 Julai mwaka 1918 na aliaga dunia tareheh 5 Disemba mwaka juzi. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limetangaza tarehe 18 mwezi Julai kila mwaka kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela kutokana na kujitolea kwake katika kueneza utamaduni wa amani duniani kote. Mzee Nelson Mandela alifungwa jela miaka mingi na utawala wa Wazungu wa Apartheid kutokana na kupigania haki za raia weusi wa Afrika Kusini.

(chanzo tehran radio udhaa ya kiswahili)
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :