Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anafanya mazungumzo mjini Washington na rais wa Marekani Barack Obama.
Mazungumzo baina ya viongozi hao wawili yanalenga ushirikiano katika vita dhidi ya wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Buhari pia ameahidi kushughulikia ufisadi
Awali Marekani ilikubali
kuisaidia Nigeria katika vita dhidi ya makundi ya uasi hasa baada ya
kutekwa nyara kwa wasichana zaidi ya 200 wa shule kutoka Chibok mwaka
jana.
Mazungumzo hayo yatajumuisha uwezekano wa msaada wa kukabiliana na Boko Haram
Hata hivyo uhusiano baina ya
Marekani na utawala ulioondoka madarakani wa Goodluck Jonathan
ulidhoofika , baada ya shutuma za makundi ya kutetea haki za kibinadamu
kuhusu ukiukaji wa haki za kibinadamu unaotekelezwa na jeshi la Nigeria.
Bwana
Buhari pia ameahidi kushughulikia ufisadi na amesema atarejesha
mabilioni ya dola yaliyofichwa kwenye benki za Marekani Uswiss na
kwingineko.
NI MWANDISHI WA TOP NEWS BLOG, AMESHAFANYA KAZI YA UANDISHI NA UTANGAZAJI KATIKA KITUO CHA RADIO-PANGANI FM RADIO,LAKINI KWA SASA ANAENDELEA NA ELIMU YA JOURNALISM KATIKA NGAZI YA DIPLOMA-MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO-TANZANIA
Post A Comment
Hakuna maoni :